WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Wednesday 16 November 2016

TAHADHARI: WIZI MTANDAO KUONGEZEKA KUELEKEA MWISHO WA MWAKA

Unapo wadia mwisho wa mwaka wizi kupitia mtandao umekua ukishika kasi zaidi – Mataifa mengi duniani yamekua yakikumbwa na wimbi kubwa la uhalifu mtandao unao ambatana na upoteaji wa pesa. Itakumbukwa mwaka jana kuelekea mwisho wa mwaka ndio kirusi kipya aina ya ModPOS kilionekana kwa mara ya kwanza na kilifanikiwa kudhuru maeneo mengi na kusababisha kiasi kikubwa cha fedha kupotelea mikononi mwa wahalifu.

Mwezi huu wa kuminamoja pekee tayari kumekua na matukio mengi yenye mlengo wa kuwapatia pesa wahalifu mtandao. Kwa sasa Uhalifu mtandao kpitia kirusi cha RANSOMWARE kinachoendelea kushikakasi wamefanikiwa kupata mamilioni ya fedha. Kirusi hiki kinapelekea mhalifu mtandao kumfungia uwezo mmiliki halali kutumia kifaa chake akimtaka alipe kiasi cha pesa ili kurudishiwa huduma. Uhalifu huu umepiga hodi Barani Afrika na hadi sasa wengi wameendelea kua waathirika.

Mifumo ya hospitali, mashule na watu binafsi ni miongoni mwa waathirika wa kubwa wa uhalifu huu ambapo kila mfumo ulio fungiwa na kirusi cha Ransomware ili kufunguliwa kiasi cha dola Miatatu (300) na zaidi kimekua kiki hitajika. Kupitia matukio yaliyo ripotiwa duniani kote, takwimu halisi ya pesa zilizo ingia mikononi mwa wahalifu mtandao kwa mwezi huu wa kuminamoja pekee kutokana na Ransomware bado haija patikana ingawa ina kadiriwa kuzidi dola milioni 829.

Aidha, Mabenki nayo hayako salama – Idadi ya Mabenki yaliyo vamiwa kimtandao imeendelea kukua zaidi kuanzia mapema mwezi huu huku hali hii ikitegemewa kuendelea zaidi maeneo mengi. Tukio kubwa zaidi kwa sasa ni kutokea uingereza ambapo hadi sasa benki ya Tesco baada ya kushambuliwa kimtandao zaidi ya Paundi milioni mbili zimeweza kupotelea mikononi mwa wahalifu mtandao na benki hiyo imelazimika kuwalipa wateja wake.


Urusi nayo, kwa mwezi huu pekee kumekua na idadi kubwa ya mabenki yaliyo vamiwwa kimtandao. Kwa undani wa hili taarifa ya awali inaweza kusomeka HAPA  – Imezungumzwa ya kua uchunguzi unafanywa, Uchunguzi unategemea kueleza kama mashambulizi mtandao yaliambatana na kuibiwa kwa fedha kwenye mabenki husika taarifa mpya zinaelezea hofu ya kua kuna kiasi kikubwa cha pesa kitakua kimepotea pia inayo mabatana na hasara ya huduma kukosekana kutokana na mashambulizi hayo.


Changa moto kubwa tulio nayo kutoka taasisi za kifedha ni kutopokea taarifa na wakati mwingine matukio yanapo kua makubwa taarifa inayotolewa inakua si sahihi – Inaficha uhalisia wa ukubwa wa tukio kitu ambacho kinapelekea wahalifu mtandao kuendelea kushika kasi.

Mitandao yasimu hasa barani Afrika ambapo huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu inapatikana, napo kumekua na aina nyingi ya wizi mtandao amabapo matukio ya watu kuibiwwa pesa yame endelea kushika kasi.

Kuna matukio mawili kwa kipindi hiki yamejitokeza nitayatolea mfano hapa ili kukuza uelewa kwa watumiaji mitandao ya simu kua makini :–

Tanzania: Nilifahamishwa na mtu ninae mfahamu mwenye huduma za uwakala wa fedha kupitia mitandao ya simu ambapo alinieleza, kwaufupi – Alikua akiwasiliana na mtu kupitia simu akimueleza ni mhusika kutoka kampuni moja ya simu nchini na kwenye mawasiliano aliyo eleza alikua akiamini kabisa ni mtu sahihi yalikamilika kwa mhusika kupoteza kiasi cha zaidi ya Milioni saba za kitanzania.

USHAURI KWENYE HILI: Kwanza kabisa, tuwe na tabia ya kujihakikishia tunao wasiliana nao ni watu sahihi hasa linapo kuja swala la fedha kuhusika. Unaweza kulifanya hili kwa kuwasiliana moja kwa moja na huduma kwa wateja au kwenda kwenye mtandao husika kabla ya kufanya muamala wowote.

Kenya: Kuna mtu mmoja nae namfahamu, alipigiwa simu na mtu alio mfahamisha anatatizo la laini yake kusajiliwa mara mbili. Katika mazungumzo yao katika simu alijikuta akitoa taarifa zake binafsi na baadae kujikuta amepoteza pesa zote alizo kua amehifadhi katika simu yake.  Kiasi ambacho ni cha takriban laki tisa za kitanzania.

USHAURI KWENYE HILI: Kwanza kabisa, Hakikisha hutoi taarifa zako binafsi kupitia simu. Makampuni ya simu yana jukumu la kuji hakikishia mhusika anaye jaribu kutengeneza laini yenye namba inayo tumika ni sahihi ( kwa Tanzania tumepiga hatua kwenye hili, tumekua na mikakati ya kuzuia watu kutengeneza laini ambazo zimetumiaka “Swapping” na tayari nimeshauri maka mpuni ya Kenya kua natabia hii) Hii ni njia pekee ya kukabiliana na tukio kama hili.

Kwa wastani Barani Afrika, Matukio kama niliyo ainisha kwenye mifano miwili hapo juu yaliyo ripotiwa kwa mwezi huu pekee yanaelezwa kupanda kwa asilimia 12.7 kulinganisha na miezi 6 iliyopita. Takwimu hizi ni kubwa sana na ni lazima elimu sahihi ya uelewa “Awareness” itolewe kwa watumiaji ambapo jukumu hili linatakiwa liwe la mitandao ya simu.

Kwenye hili la elimu ya uelewa, Nimeshuhudia Vipeperusi vinavyo tolea ufafanuzi wa kuhakiki mtumiaji huduma za kifedha kupitia simu anabaki salama na fedha zake ambavyo nilirizishwa navyo  Nchini Kenya – Tanzania tunavyo vipeperushi pia vinavyo bandikwa kwa mawakala lakini bado havina taarifa za kutosha.

Aidha, Kwa nchi zote zenye kutumia huduma za fedha kupitia mitandao ya simu ni lazima vielewe vipeperushi vinavyo bandikwa kwa mawakala pekee havitoshi lazima kuwe na njia nyingine nzuri ya kukuza uelewa wa watumiaji ili kulinda fedha zao wanapo ziifadhi kupitia simu zao za mkononi.


Niendelee kutoa wito, Jukumu la ulinzi mtandao lazima lianzie katika ngazi ya mtu binafsi. Aidha, Lazima tuwe na tabia ya kuripoti matukio haya ya kihalifu mtandao ili yapatiwe suluhu. Ni vigumu kukabiliana na uhalifu huu kama hakuna taarifa zinazotolewa. Pia ni lazima tuwe na tabia ya kua na tabia ya kuzuia tatizo pasi na kungoja litokee ndio tuhangaike kutafuta suluhu.                     


Mataifa ya Afrika lazima yashirikiane kukabiliana na uhalifu mtandao, Sheria mtandao ziwe zina wiana ili kuweza kufanya kazi maeneo yote, tuhakiki tunakua na watu sahihi wenye uwezo sahihi wa kukabiliana na uhalifu mtandao pamoja na kuwekeza kwenye vifaa vya uthibiti uhalifu mtandao – Elimu ya uelewa pamoja na kuwaongezea watu wetu ujuzi mara kwa mara ya maswala haya ya usalama mtandao.

No comments:

Post a Comment