WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Sunday 9 October 2016

UWEKEZAJI SEKTA YA TEHAMA UANGAZIE USALAMA MTANDAO

Mataifa mbali mbali yame endelea kuwekeza katika sekta ya TEHAMA ikiwa ni katika jitihada za kurahisisha upatikanaji wa mawasiliano kwa wanchi wake pamoja na kukuza ufanisi katika utendaji kupitia utumiaji wa mifumo ya Digitali/Tehama.

Teknolojia ya Setilaiti imeongeza chachu kwenye hili na kwa kuliangalia hili Jijini Addis Ababa Nchini Ethiopia mkutano wa kwanza kwa nchi za Africa wenye kauli mbiu “Digital Skies – Everyone connected”  ulipata kujadili kwa kirefu maswala mbali mbali yahusuyo TEHAMA ambapo Viongozi mbali mbali na wataalam katika nyanja hii walipata kuwasilisha mada na kushiriki katika mijadala mbali mbali.

Waziri wa TEHAMA wa Nchi ya Somalia Mh. Jamal Hassan alikua ni mingoni mwa walio zungumza, ambapo ali ainisha TEHAMA inavyo endelea kukua kwa kasi nzuri katika taifa lake.

Mwanzo wa kuwasilisha mada yake alianza kwa kusema, Somalia imekua na umaarufu mkubwa katika maswala ya ugaidi, Lakini Nchi imepiga hatua nzuri katika kuwekeza katika sekta ya TEHAMA.

Akifafanua alieleza taifa lake (Somalia) linatumia huduma ya fedha mtandao na fedha kupitia simu ambapo wafanyakazi wake wana endelea kulipwa kupitia simu za mkononi. Aidha, Aliainisha mifumo mbali mbali imeendelea kuwa ya kidigitali ili kuhakiki ufanisi unakua.

Aliongeza kwa kusema wananchi wa taifa hilo wameendelea kua na matumizi makubwa ya mitandao ikiwepo mitandao ya kijamii inayo rahisisha mawasiliano baina yao. Alizungumza pia mpango wa Nchi yake kupata huduma ya Mkonge ambao alisema utatokea Dar-es salaam hadi Nchini mwake.


Kwa ufupi alianisha jitihada mbali mbali ambazo, pia taifa la Tanzania limeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa na tayari kama taifa tumepiga hatua kubwa sana.

Baada ya kuwasilisha mada yake nilipata kufanya nae mazungumzo waziri huyo wa Somalia, ambapo kwanza nilimpongeza kutokana na ukweli kwamba sikua nafahamu mengi aliyo yazungumza na sikuwahi kudhania kutokana na mengi tunayo yasikia kutoka kwenye taifa hilo.


Lakini pia, Nilionyesha wasi wasi wangu kwake na kunukuu ripoti ya usalama mtandao ya mwaka huu ambayo tayari nilisha ijadili na kumwambia ilionyesha taifa lake ni miongoni mwa nchi zinazo athirika zaidi na mashambulizi mtandao/ Uhalifu mtandao katika ngazi ya kidunia.

Nikamuuliza nchi yake ina mikakati gani kukabiliana na hali hiyo – Aliita watendaji wengine akiwemo katibu mkuu wa wizara yake na Mkuu wa kampuni ya simu ya nchi hiyo ili kuweza kuzungumzia hili.


Nilicho gundua katika mjadala wangu na wao ni kwamba kama ilivyo katika mataifa mengine barani Afrika, Uwekezaji katika sekta ya TEHAMA hauendani sambamba na usalama wake kitu ambacho kimeendelea kusumbua mataiffa mengi ya kiafrika.

Mwisho wa mazungumzo yetu , Waliamua kunialika Nchini mwake na wali nitaka katika matembezi yangu niweze kutazama walicho fanya na kuwashauri zaidi katiaka sekta ya usalama mtandao. Mwaliko  ambapo nili muahidi kujitahidi kutafuta wakati na kutembelea Taifa hilo.

Mada nyingine ni ya Gavana wa Kauti ya Bungoma, Kenya Mh. Kenneth Lusaka ambapo iliweza kufafanua vizuri umuhimu wa mataifa kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya TEHAMA ambapo kama walivyo zungumza watangulizi wengine ali weza kuainisha hatua kubwa  ambayo Kaunti anayo iongoza imepiga  katika sekta ya TEHAMA huku akitolea mfano wa mfumo wa ukusanyaji mapato kupitia TEHAMA ambapo alieleza umeongeza situ ufanisi bali uwazi na umechangia kupunguza rushwa kwani kila fedha inayo ingia inaonekana kwenye mfumo wa kidigitali.

Aliongeza na kusema ukuaji wa Teknolojia hii lazime uangazie pia tishio kubwa la uhalifu mtandao ambapo lazima upatiwe suluhu ya kudumu. Wahudhuriaji wa mkutano walionyesha kufurahishwa sana na hotuba yake hasa alipo zungumzia swala la usalama mtandao.

Binafsi, Nilishiriki katika mkutano huu na nikapewa heshma ya kuongoza moja mjadala ambapo uliangazia usalama mtandao – Kimsingi dhana kuu ya mjadala nilioshiriki ilikua situ kukumbusha kua tunapo endelea kuunganisha kila mtu na kuwekeza zaidi katika sekta ya TEHAMA inayo endelea kuturahishia mambo mbali mbali mbali pia unaongeza  kasi ya uhalifu katika mitandao. Aidha, mjadala  pia  uli jikita katika kutoa ushauri wa nini kifanyike.

Nikizungumza nilitolea mfano  vyombo vya usafirishaji (mfano: Magari, Treni na Ndege) vinavyoweza kuangushwa kupitia uhalifu mtandao na nikaelezea tukio la magari Milioni 1.4 aina ya JEEP yaliyo lazimika kurudishwa kiwandani baada ya kuweza kuangushwa na wahalifu mtandao.

Aidha, nilizungumzia tukio la mifumo ya umeme ya Nchi ya Ukrine iliyoweza kuzimwa na wahalifu mtandao, Pesa zinazopotea kwa kasi kupitia uhalifu mtandao na taarifa mbali mbali zinavyo endelea kuinbiwa kupitia mtandao huku tovuti na mifumbo mbali ya kidigitali inavyo angushwa kila siku na wahalifu mtandao.

Niliendelea na kusema pamoja na hali hii kuwa ni ya kutisha wana usalama mtandao duniani kote tumeendelea kutafuta suluhu ya matatizo na kuendelea kushauri matafa mbali mbali juu ya nini cha kufanya ili kuendelea kubaki salama kimtandao.

Kiujumla mkutano ulikua ni wenye faida kubwa na tumekubaliana kufanyia kazi tuliyo yazungumza na pia binafsi nikitegemewa ikiwa ni moja ya makubaliano kuweza kuzuru mataifa kadhaa ili kuweza kuimarisha mashirikiano katika swala la kukabiliana na uhalifu mtandao.


HABARI NJEMA: Tanzania kupitia Chuo cha Nelson Mandela cha Arusha ambapo pia niliweza kukitembelea hivi karibuni kipo katika hatua nzuri ya kuanzisha mafunzo ya usalma mtandao katika ngazi ya shahada ya pili (Masters) ambapo ni katika kuhakiki kama taifa tunaendelea kukuza wataalam wetu wa ndani – Jambo ambalo kwa muda nilikua nikiomba chuo hicho kiweze kutoa mafumzo hayo na nimefarijika kuona Januari huwenda yakanza kama kila kitu kitaenda sawa.



No comments:

Post a Comment