WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday 26 August 2016

UHALIFU MTANDAO NA ATHARI KIUCHUMI

Yapo maeneo mengine ambayo yanaweza kuathiriwa vibaya na uhalifu mtandao – UCHUMI, ni moja ya eneo muhimu ambalo wahalifu mtandao wanaweza kuliletea athari. Aidha, Unapotazama kinacho wapelekea wahalifu mtandao kufanya uhalifu moja wapo ni kujipatia fedha.

Ni wazi kua Raisi wa awamu ya Tano ana pambana kwa dhati kuhakiki wa Tanzania wanaondokana na umasikini ulio kithiri ambapo anaendelea kuchukua jitihada na hatua mbali mbali hadi sasa.

Mfano: Kumekua na uhimizaji mkubwa wa ukusanyaji wa kodi ki elektriniki – Kwa njia ya mtandao ambapo amesisitiza anataka aone TEHAMA inatumiwa vizuri katika eneo hili ili kuhaliki hakuna upotevu wa pesa katika ukusanyaji wa kodi Nchini.

Aidha, Mabenki yameendelea kuboresha mifumo ya Kimtandao kuhakiki miamala inafanyika zaidi kupitia mtandao na nikitolea mfano, mabenki Nchini yamekua yaki hamasisha huduma mtandao kama vile (Huduma za kifedha kupitia simu, kutumia kadi zetu kufanya manunuzi pamoja na matumizi ya mashine za kutolea fedha “ATM”)

Makampuni ya simu nayo hayajakubali kubaki nyuma – Yame hakiki yanaingiza huduma inayoshika kasi zaidi Nchini ya kuweza kufanikisha miamala ya kifedha kupitia simu zetu (Mobile money) ambapo wana nchi wengi wameendelea kuona huduma hizi ni rahisi na wengi wanazitumia.


Maeneo mengine nayo yameona huu ndio muelekeo – Mabasi ya mwendo kasi yamehamasisha miamala kufanyika kwa kadi, huku ulipaji wa bili mbali mbali nao kuendelea kufanyika kupitia mitandao.

Hali hii ni nzuri sana – Kitendo cha mtu kuweza kufanya miamala ya kifedha bila kuhangaika kutoka shemu moja kwenda nyingine kunapelekea uokoaji wa muda na kuongeza ufanisi kwa tunayo yafanya. LAKINI – Je, Upande wa pili wa shilingi, kuna jitihada zozote tumechukua kuangazia? Hapa nazungumzia wahalifu mtandao ambao pia wana uwezo mkubwa wa kupelekea upotevu mkubwa wa pesa tunazozizungusha mitandaoni.

Ni mara ngapi tumekua tukiathirika kimtandao kunapo pelekea kupoteza pesa zetu, bila kujadiliwa kwa sura ya kipekee? Kuna wanao lalama bila kufata taratibu juu ya kupotelewa kwa fedha, na kuna wanao potelewa bila kujua na pia kuna wanao dai wametoa taarifa lakini hakuna matokeo chanya.

Taasisi za kifedha nazo si kweli kua hazi kubwi na kadhia ya upotelewaji wa fedha kupitia mitandao, Lakini ni Aghalab kusikia haya yakizungumzwa na kujadiliwa kwa kina.


COSTECH iliandaa mkutano uliokutanisha watafiti na wana sayansi katika fani mbali mbali nchini ambapo ulidumu kwa siku tatu – Kutokana na sababu kadhaa, Nilifanikiwa Kushiriki vikao hivyo katika masaa ma chache ya mwisho pekee ambapo mjadala wa maswala ya usalama mtandao ulifanyika na mambo mengi ya msingi kujadiliwa.

Kwa mujibu wa Tafiti zilizo wasilishwa na AARSC kwenye moja ya mjadala, zime eleza asilimia sita (6%) pekee ya tovuti nchini ndizo zenye ulinzi mtandao unao ridhisha na Asilimia kumi na tisa (19%) zipo katika hatari zaidi ya kuweza kuvamiwa na wahalifu mtandao.

Aidha, Asilimia zilizo bakia, sabini na tano (75%) zipo katika hali mbaya kwa kiwango cha wastani sanjari na kiwango kidogo – Ambapo pia zinabaki kua katika hatari ya kuweza kuingiliwa na wahalifu mtandao. Mjumuiko wa takwimu hizi ni pamoja na tovuti za mabenki yetu Nchini.

Muwasilisha tafiti aliendelea na kusema, Kilicho ikumba benki ya Bangladeshi – Mapungufu yaliyo patikana yana wiana pia na mapungufu yaliyo patikana kwenye tovuti za kwetu nchini. Beki ya Bangladeshi iliweza kuingiliwa na wahalifu mtandao na kupelekea upoteaji wa kiasi kikubwa sana cha pesa. Unaweza kupitia kwa kirefu kuhusiana na tukio la Benki ya Bangladesh kwa ku “BOFYA HAPA”

Aidha, kwenye hitimisho la tafiti iliyo wasilishwa iliainisha – Kwa uumla hali ya tovuti zetu nchini ni mbaya. Kitu ambacho kilinifanya nijiulize maswali kadhaa. Wachangia mada walitolea mfano shambulizi mtandao la hivi karibuni katika Chuo cha IFM pamoja na kampuni ya simu ya TTCL.

MASWALI YA MSINGI

Kuna maswali mengi mtu anaweza kujiuliza, Mfano: Matukio haya ya kihalifu mtandao wa Tanzania huwa wanajua kinacho endelea? Tatizo hasa liko wapi? Nini kifanyike? Pamoja na maswali mengine mengi.

Sitaki kutupa lawama moja kwa moja kwa walio nyuma ya utengenezwaji wa tovuti pamoja na wasimamizi wake Nchini – Huwenda swala la usalama mtandao bado ni JIPYA kiasi kwamba inakua vigumu kuweza kufahamu mapungufu ya kinacho tengenezwa (Tovuti na mifumo mingine).

Au Inawezekana ikawa kuna changamoto ya kuzungumzia udhaifu tulio nao katika mifumo yetu kutokana na sababu mbali mbali. Najiuliza, Kama hili ni kweli – hatuoni tunachofanya ni sahihi hasa ulizingattia Uchumi wa taifa lolote duniani unaweza kuyumbishwa vibaya na wahalifu mtandao?


Katika kujibu maswali tunayoweza kujiuliza – Naweza kusema, Uelewa bado uko chini sana wa maswala haya ya uhalifu mtandao ( Hapa namaanisha utambuzi, Kujilinda pamoja na hatua za kuchukua tatizo linapo tokea) Hii ni kuanzia ngazi ya mtu binafsi hadi ngazi ya Kitaifa.

Ni wazi kuna tatizo kubwa, na hili si tatizo la taifa moja ni tatizo la kibara na kidunia. Kubwa kuliko yote ni kua tumekua na wadhibiti dhaifu kuliko wahalifu mtandao na hatuna miundo mbinu rafiki ya kuhakiki tuna tumia rasili mali watu vizuri kwa kuzitambua na kuhakiki zinabaki upande salama badala ya kuwa wa halifu. Hii ni moja kuu lakini bado kuna sababu nyingine 11 mbazo katika nyakati tofauti nimekua niki zielezea.

Kinachotakiwa kufanyika, Kikubwa ni kua na UTAMBUZI wa changamoto za uhalifu mtandao pamoa kua na UTAYARI wa kuzitatua na kuhakiki mapendekezo tuliyo kubaliana (wana usalama mtandao ) na kuyapitisha tulipo kutana ijini Johannesburg Nchini Afrika kusini  ambayo mataifa mengine sasa yako katika kuyafanyia kazi nasisi tuna yafanyia kazi kama taifa.

JITIHADA NYINGINE – TEHAMA

Ni ukweli ulio wazi kua, TEHAMA ina mchango mkubwa sana wa kuondoa umasikini kwa watanzania – Na bahati nzuri kitabu kilicho zinduliwa mwisho wa mkutano “ICT pathway to Poverty reduction” kinaelezea vizuri hili.

Katika utambuzi wa manufaa makubwa ya matumizi ya TEHAMA, Taifa limewekeza vizuri kwenye maswala ya TEHAMA – Nikitolea mfano michache, naweza kuzungumzia mkonge wa taifa, Ghala la taarifa la taifa “National Data Centre”, na mifumo mbali mbali yaki TEHAMA inayotumika katika miamala ya kifedha Nchini.

Aidha, bado kuna jitihada pamoja na ahadi kadhaa za kuendelea kuwekeza zaidi katika TEHAMA nchini ili kurahisisha maisha ya watanzania na kuhakiki kila mmoja wetu ana nufaika kupitia TEHAMA ikiwa ni miongoni mwa vichocheo vya kutupeleka katika Uchumi wa Kati sanjari na kua taifa la viwanda.

Sekta ya Afya imeendelea kujikita katika matumizi ya TEHAMA (Mfano: Telemedicine) – Nimetolea ufafanuzi wa taarifa ya hivi karibuni tuliyo jadili ya changamoto za TEHAMA katika sekta ya Afya kupitia andiko linaloweza kusomeka kwa ku “BOFYA HAPA” ambapo ninaamini kuna mengi tunaweza kujifunza na kuzingatia.




No comments:

Post a Comment