WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday 31 March 2016

ONGEZEKO LA UHALIFU MTANDAO NI ZAO LA ULINZI MTANDAO DHAIFU AFRIKA

ANGOLA Imekumbwa na Shambulio la kimtandao kutoka katika kundi la wahalifu mtandao wajulikanao kama “Anonymous”  ambapo tovuti 20 za serikali ya Nchi hiyo zimefanikiwa kuangushwa na kundi hilo la kihalifu mtandao.

Tukio hilo lilitokea kufuatia shinikizo la kuachiwa huru watu 17walioshikiliwa nan chi hiyo kutokana na kosa la  wakipingana na uongozi wa raisi wa Nchi hiyo Mh. Jose Eduardo dos Santos.

Tukio hilo la kushambuliwa kwa tovuti za Nchi ya Angola limepokelewa kwa Maskitiko makubwa sana na wana usalama mtandao wa Nchi za Afrika na imeonekana changamoto iliyojitokeza iwe ni funzo kua mataifa ya afrika bado yanahitaji jitihada za dhati kuhimili vishindo vya wahalifu mtandao.

------------------------
NEWS UPDATES: A Portuguese branch of the Anonymous hacking group says it has shut down about 20 Angolan government websites in retaliation for the jailing of 17 youth activists for plotting a rebellion against President Jose Eduardo dos Santos' government.
-------------------------
GHANA ilipata kuathirika na tukio la kuangushwa tovuti zake mwaka jana kitu ambacho kilipelekea Nchi hiyo kupitia Makamu wake wa Raisi kujipanga zaidi kuhimili vishindo vya kihalifu mtandao.Taarifa zaidi kuhusiana na tukio la Ghana inasomeka kwa ku “BOFYA HAPA”


TANZANIA Imepata kuathirika na tatizo la kuingiliwa tovuti kadhaa kipindi cha nyuma na kusababisha tovuti husika kushindwa kutoa huduma na mara nyingine kuingiziwa vitu visivyo faa.

KENYA Pia Ilipata kuathirika kwa kiasi kikubwa kwa tovuti zake kitu kilicho sababisha baadhi ya tovuti kufungwa moja kwa moja – Tulipata kujadili hili kwa kina nilipo udhuria mkutano wa usalama mitandao wa Nchi za Afrika mashariki uliofanyika mwaka jana  nchini Kenya.

UGANDA, kuimarisha amani ya nchi hiyo kipindi cha uchaguzi mwaka Huu ililazimika kufunga mitandao yake ya kijamii pamoja na mifumo mingine ya kimtandao ikiwa ni hofu ya amani kuyumba. Huu ni mfano ulio hai wenye mazingatio makubwa ndani yake.

AFRIKA  kwa ujumla wake matukio kadhaa yamepata kutokea nabado yame endelea kutokea  ambapo ni zao la kutotiliwa mkazo swala zima la ulinzi mitandao kwa Nchi zetu barani Afika kitu ambacho nadhani imefika wakati pakatiliwa manani mapendekezo ambayo yamekua yakitolewa ili kuweza kubakisha bara letu salama kimtandao.

DUNIANI kote kumeendelea kuzaliwa  makundi lukuki ya Kiahalifu mtandao amabapo yameendelea kusababisha maafa makubwa maeneo mbali mbali Duniani – Mfano Kundi la “Carnabanak” tayari limefanikiwa kuiba ma bilioni ya kimarekani hadi sasa kwa mujibu wa Ripoti iliyo wasilishwa mapema mwaka huu.

Uchumi, Utamaduni, Siasa, Upatikanaji wa Huduma Muhimu ni kwa uchache tu wa mambo ambayo yameendelea kuathirika kwa kiasi kikubwa kupitia uhalifu mtandao.

Juhudi mbali mbali bado zinaonekana ingawa kiujumla wake Nchi za Afrika bado zimeonekana kutoa uzito mdogo sana kukabiliana na tishio kubwa la uhalifu mtandao.
Kumekua na baadhi ya Nchi za Afrika zilizo fanikiwa kuwa na Sheria mitandao ambapo baadhi bado zimeendelea kua na changamoto. Kuwapo na Sheria pekee bado imekua ni changamoto kwani vinavyo takiwa kwenda sambamba na sheria hizo ili kuweza kufikiwa malengo tarajiwa bado havitiliwi uzito.

Hili limesababisha uhalifu mtandao kuendelea kutikisa na kuathiri jamii zetu huku baadhi kushindwa kujua  athari hizi zinaweza kupelekea mambo mengi kujitokeza. Kuyumba kwa Uchumi, Kupoomoka kwa maadili, kutikisika kwa amani na Kutopatikana kwa huduma muhimu zinapo hitajika ni miongoni tu kwa uchache kwa kinachoweza kuleta shida ndani ya mataifa yetu ikiwa ni zao la kukithiri uhalifu mtandao.

Bado imekua ni aghlab kusikia wakuu wa Nchi za Afrika kuzungumzia maswala ya usalama mitandao isipokua tu pale wanaposhiriki makongamano ya kiusalama mitandao.


Natoa wito kwa Nchi zetu za Afrika kuhakiki zinawekeza zaidi kulinda mifumo yetu ya kitehama ili kuweza kusababisha athari kubwa zinazotokana na uhalifu mtandao kutoshika kasi kama ilivyo sasa.

No comments:

Post a Comment