WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday 18 February 2016

TAARIFA BINAFSI ZA WANACHUO ZA ANIKWA MTANDAONI

Matukio yaki halifu mtandao kwa mwaka huu wa 2016 yameonekeana kushika kasi zaidi ya ilivyotegemewa. Tayari kumekua na matukio kadhaa ya kihalifu mtandao ambapo baadhi yao watoto wa umri kati ya miaka Tisa (9) na Kumi na saba (17) wanahusika.

Hali hii pamoja na tishio la makundi ya kihalifu mtandao kutishia kuyumbisha UCHUMI wa mataifa mengi duniani imepelekea wana usalama mtandao kuzidi komba mataifa mbali mbali kujipanga zaidi kukabiliana na uhalifu mtandao.

Mapema Mwezi huu, taarifa binafsi za wanavyuo wa chuo cha Greenwich zimeonekana kusambazwa  mitandaoni. Kufuatia mamia ya taarifa za wanachuo hao kupatikana mtandaoni, Chuo hicho kimeomba radhi na tayari chuo hicho kinaendelea kuwasiliana na wanachuo wote walio athirika na tukio hili. Wakati huo huo tukio hilo limeripotiwa na upelelezi bado unaendelea.

Uchunguzi wa awali umeonyesha huwenda wadukuzi walifanikiwa kuingilia mifumo ya chuo hicho na kusababisha taarifa hizo binafsi kusambaa mitandaoni. Tukio hili linafatia tukio la kijana wa miaka 16 kudukua mifumo ya vyombo vya usalama Nchini marekani pamoja na barua pepe ya mkurugenzi wa CIA ambapo taarifa zilizopatikana huko pia zili anikwa mitandaoni.

Wanasheria wameonya tukio hilo linaweza kuligharimu chuo hicho pesa nyingi endapo wana vyuo hao watashitaki kutokana na taarifa zao binafsi walizo zipatia chuo hicho hazikupatiwa ulinzi wa kutosha na hatimae kuishia mikononi mwa wahalifu mtandao.

Miongoni mwa taarifa za wanachuo zilizopatikana mitandaoni ni pamoja na majina yao, Namba zao za simu, Miaka yao ya kuzaliwa, Mahli wanapo ishi, Sahihi zao, taarifa zao za hospitali (medical history) pamoja na mambo mengine.


Kwa sasa Taarifa hizo zime ondolewa mtandaoni na chuo hicho kimesha fanya mawasiliano na Google kuhakiki taarifa hizo haziendelei kuonekana kupitia kisakuzi cha google.

----------------------------------------------------------
NEWS UPDATES: Computer systems at the Hollywood Presbyterian Medical Center in southern California have fallen prey to ransomware. The systems have been offline for more than a week. Employees were not able to access patient files and the hospital declared the situation an internal emergency. The FBI, the Los Angeles Police Department, and cyberforensics experts are investigating. The attackers have demanded a ransom of 9,000 Bitcoins (approximately US $3.6 million; 3.2 million euros.)
--------------------------------------------------------------

Aidha, Ripoti iliyokua ikingojwa ya “Horizon scan” iliyokua ikiandaliwa na taasisi ya maendeleo ya biashara, BSI imetoka. Ripoti hiyo iliyo fanywa kwa kukusanya maoni kutoka kwa mashirika makubwa kujua hofu yao kubwa inayo ikumba makampuni ni ipi kwa mwaka huu wa 2016 imeonyesha makapuni mengi yanahofu na uhalifu mtandao ambapo wanaamini kuna uwezekano mkubwa uhalifu huu kuyumbisha ukuaji na kuendelea kwa makampni mbali mbali.

Imeainisha makampuni yameendelea kuingiwa na hasara mara kwa mara baada ya wahalifu mtandao kufanikiwa kuiba fedha nyingi na kusababisa kuyumba kwa ukuaji wa mapato.

Kwa miaka miwili mfululizo uhalifu mtandao kuonekana kushika nafasi ya kwanza katika ripoti ya taasisi hiyo.

---------------------------------------
QUOTE: A total of 48% of respondents said they were “extremely concerned” this year about the possible threat of a cyberattack impacting their company, such as a malware or denial of service incident. Second on the list of top threats this year was a data breach, with 41% of respondents saying they were “extremely concerned.” Unplanned IT and telecom outages came in third, with 35% saying they were extremely concerned about the threat.
-----------------------------------------

Aidha, Kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA kunapopelekea ukuaji wa uhalifu mtandao duniani kote kumepelekea mataifa mengi kua na mikakati madhubuti kukabiliana na hatari ya wahalifu mtandao kuleta athari katika Nyanja zote hasa kiuchumi.


Kufuatia hili Nchi ya Marekani kwa mara ya kwanza ameweza kuwasilisha bajeti ya Dola Bilioni 19 za kimarekani ili kukabiliana na tishio kubwa la uhalifu mtandao huku ikiimarisha azimio la ushirikiano wa vitengo vinavyohusika na kupambana na uhalifu mtandao nchini humo.

No comments:

Post a Comment