WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Sunday 21 June 2015

UHALIFU MTANDAO KUELEKEA UCHAGUZI 2015

Nianze makala hii kwa kupongeza jitihada za dhati za serikali ya awamu ya Nne katika uwekezaji wake kwenye sekta ya TEHAMA Nchini. Ni wazi kabisa nchi yetu imepiga hatua kubwa katika maswala ya TEHAMA kulinganisha nan chi nyingi Afrika. Mifano michache ni pamoja na kuhama kutoka analogia kulekea Digitali, Mkonge wa taifa, Kupatikana kwa Khala Mtandao la taifa, kuaandikisha upigaji kura kimtandao na mengineyo mengi.

Aidha, Jitihada kama vile kupatikana kwa sharia mtandao, kupatikana kwa vitengo vinavyo shughulikia uhalifu mtandao,  wakala za serikali mtandao na mengineyo yamekua ni hatua ya kipekee iliyoweza kutoa matumaini kwa watanzania kutoka kwa serikali ya awamu hii ya Nne inayo ongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.

Jitihada hizi njema naona bado kuna ya kufanyika zionyeshe matunda na zibaki salama kwa muda mrefu. Nimeyasema hayo kufuatia kauli yangu niliyoitoa, Nilipo sema serikali ina jukumu la kuwekeza zaidi katika maswala ya usalama mitandao ili kuweza kubakisha salama jiihada hizi za TEHAMA kwani isipo fanywa hivyo kuna hatari kubwa mbele yetu kimtandao iyakayo pelekea jitihada hizi kuingia dosari kubwa.

Hatari za kimtandao zitakazo pelekea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wetu, siasa zetu, tamaduni na jamii yetu kwa kwa ujumla wake. Napo zungumzia uchumi nipamoja na upotevu mkubwa wa fedha unaosababishwa na uhalifu mtandao ulio athiri taasisi za fedha na mawasiliano nchini. Kumekua na wimbi kubwa la wizi wa fedha kimtandao hii ni mjumuisho wa pesa kutoka mabenki pamoja na pesa zinazo potea kutokea kwenye miamala ya simu.

Moja ya changamoto iliyo sikika kwenye kikao nilichoshiriki kilicho husisha nchi ya  ujerumani na Tanzania ni pamoja na lalamiko kutoka kwa mshiriki kuelezea kua kupitia mtandao alipoteza pesa zake na kumekua na ugumu kuzipata pesa hizo. Nilitolea ufafanuzi hilo kwa kueleza kua tatizo ni kubwa na kama hakuna jitihada za dhati kudhibiti hili basi kuna hatari ya uchumi wetu kupitia uhalifu huu mtandao kuporomoka.

Aidha, Naomba nijikite zaidi kwenye Uchaguzi mkuu ujao Oktoba – Ni wazi kabisa kuanzi uandikishaji hadi taratibu nyingine za kuelekea uchaguzi mkuu umehamishiwa katika mtandao. BVR (Biometric Vote Registration) mfumo mtandao unaotumika kuandikisha wapiga kura ambao kwa ujumla wake ni mfumo wwa kimtandao.

Kuna hatari kubwa ya Mifumo hii kuathirika kimtandao na kusababisha kupatikana kwa taarifa zisizo sahihi endapo wahalifu mtandao wataweza kuingilia na kufanya marekebisho wa namna ya ufanyaji kazi wake. Hii inaambapatana na Matumizi mabaya ya mitandao kuelekea uchaguzi ambapo inaweza kusababisha kuyumbisha amani iliyoko Nchini. Nimelizungumza hili kwa kirefu sana kama inavyoweza kusomeka kwa ku "BOFYA HAPA"


Ikumbukwe Wahalifu mtandao wamekua hawalali waki tafuta njia mpya za kuleta maafa mtandao na ndio maana hata baada ya kumaliza kikao maalum cha wana usalama mitandao tulipokutana Jijini Johannesburg, Ambapo Kwa ufupi taarifa yake inaweza kusomeka kwa ku "BOFYA HAPA" – Palitokea uhalifu mtandao ulio itikisa nchi ya Marekani na baadae kwenye Mahojiano yangu na kituo cha BBC nikaweza kutolea ufafanuzi walau kwa uchache ya wapi tunajikwaa kama tulivyo kubaliana mkutanoni. Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kupitia Video inayo onekana hapa.


WITO: Naomba niendelee kutoa wito katika swala zima la ushirikiano kwani taifa au kundi Fulani peke haliwezi kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao unao endelea kukua kwa kasi. Aidha, Kuendelea kukuzwa kwa uwezo watu wentu wa ndani hasa wanao shughulikia uhalifu mtandao nchini pamoja na kukukuza uelewa wa matumizi salama mitandao kwa watumiaji.


Aidha, Kupatikana kwa Chombo maalum kitakacho unganisha nguvu za vitengo kadhaa vilivyopo ili kupatikana nguvu ya pamoja kufikia malengo ya kuweka taifa letu salama pamoja na kuongeza uwekezaji katika usalama wetu wa mitandao Nchini.

No comments:

Post a Comment