WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Monday 9 March 2015

UMAKINI ZAIDI UNAHITAJIKA KWA WATUMIAJI MITANDAO.

Ukuaji wa Sekta ya TEHAMA umekuwa wa mafanikio na msaada mkubwa katika kuharakisha, kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia  kikamilifu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa letu. Kwa mfano, wananchi walio wengi sasa wanapata huduma mbalimbali za mtandao kwa kutuma na kupokea pesa; kulipia ankara za maji, umeme na tozo mbalimbali kama vile ada na leseni; na mawasiliano ya simu na intaneti pamoja na elimu mtandao na tiba mtandao.

Palipo na mafanikio hapakosi changamoto. Pamoja na kwamba tumeshuhudia manufaa na umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, biashara, miundombinu ya mawasiliano, pia kumekuwepo na changamoto ya matumizi mabaya ya mtandao katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya makundi ya watu na hata kutoka Taifa moja kwenda Taifa lingine kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni.

Baadhi ya mifano ni pamoja na  suala la wizi wa fedha kwa njia ya mtandao, matukio ya uhalifu kwa kutumia mtandao, uvujaji wa taarifa za siri, upotevu wa haki miliki na matumizi ya saini na ushahidi, mmomonyoko wa maadili, athari za makundi maalumu kama vile watoto na usalama wa miundombinu mbalimbali ya TEHAMA ambapo Serikali imeingia gharama kubwa kuiweka.

Wakati hayo yakijiri, Kwa sasa kumekua na wimbi kubwa la kurubuni watu kupitia mitandao ambapo majina ya wanasiasa, wanamuziki na wenye majina makubwa yameendelea kutumiaka vibaya katika mitandao ili kufanikisha urubuni wa kuwaibia watu pesa kwa kutumia jina la “VIKOBA” – Chakushangaza zaidi kurasa hizo zinazo onekana zaidi kupitia mitandao yakijamii zinaonekana zimedhaminiwa ili kuweza kusomwa na wengi kitu ambacho  kinapelekea kuonyesha jinsi gani wimbi hili na wahalifu hawa mtandao wamejipanga.


Watanzania hawanabudi kuwa makini sana na kuwa waangalifu sana wanapo takiwa kuingiza taarifa zao binafsi na wanapo takiwa kufata maelekezo wa kutekeleza miamala kupitia mitandao kwenye vyanzo vyenye utata.

Kumekua na malalamiko mengi kuhusiana na wimbi kubwa la watanzania waki lalamikia kuibiwa/ Kutapeliwa pesa zao kupitia mitandao ya kijamii (kwa njia ya Vikoba) liwe ni somo kwa wengine kuwa makini zaidi kwenye hili.

Aidha, Jingine linalo kuja kwa kasi ni usambazaji wa picha na maneno yasiyo rafiki kwenye mitandao ya kijamii bila na kua na uoga ya kuwa kwa kufanya hivyo inaweza kusababisha uvunjifu wa Amani katika taifa. Kwenye hili tumeshuhudia picha mbali mbali na hata maneno ya chuki, ifitinishaji na uchochezi ambayo yanatishia sana hali ya utulivu iliyopo nchini.

Bado kumeendelea kuonekana uhalifu mitandao nchini ukichukua sura tofauti mara kwa mara huku wahalifu mtandao ambao idadi ya wahalifu hao kuonekana kua ni wazawa inaongezeka kila kukicha.

Kwa mazingatio hayo ni vizuri watanzania wakatambua kua Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imechukua jukumu na kuandaa muswada wa Sheria za Matumizi Salama ya Mtandao kwa lugha ya kiingereza zinafahamika kuwa ni Cyber Laws.

Muswada wa Sheria hizo ni pamoja na muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi (The Personal Data Protection Bill); na muswada wa Sheria ya Biashara Miamala ya Ki-elektroniki (Electronic Transaction Bill) na muswada wa Sheria ya Kuzuia Uhalifu kwa Njia ya Kompyuta na Mtandao (Computer and Cyber Crimes Bills). Sheria hizi zitajikita katika masuala ya kudhibiti uhalifu kwa kutumia mitandao, udukuzi, utunzaji wa taarifa, kuwalinda watoto dhidi ya matumizi yasiyofaa ya intaneti na malipo kwa njia ya mtandao.

WITO: Sheria mtandao zinatofautiana sana na sharia nyingine kutokana na kukua na kubadilika kwa teknolojia ya habari na mawasiliano mabapo mabadiliko na ukuaji wake ni wa kasi sambamba kabisa na ukuaji na ubunifu wa njia mpya za uhalifu mtandao. Kwakuzingatia hili Sheria hizi zimekua zikipitiwa na kurekebishwa mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko husika. Ni vyema hili likatambulika ili kuhakiki sharia husika zinaingizwa katika vitendo mapema kabla ya kufikia muda wa kuzipitia il-hali bado hazijaanza kutumika.

Aidha, Kama ilivyo kwa matukio mengine yote ya uhalifu na uvunjifu wa amani katika nyanja nyingine wakati tukiendelea na uandaaji wa sheria, wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwa vyombo vya udhibiti kuhusu matukio yoyote ya ukiukwaji na matumizi mabaya ya mtandao na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kulingana na sheria na kanuni zilizopo sasa.


Mwisho, napenda kuungana na wengine kwa kutoa rai kwa wananchi wote kuwa wajiepushe na matumizi mabaya ya mitandao na badala yake watumie vizuri mitandao hiyo kwa manufaa yao wenyewe, ya jamii na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment