WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday 27 March 2015

INDIA YADHAMIRIA KUKABILIANA NA WIZI KUPITIA MASHINE ZA ATM

Katika Mkutano uliofanyika Nchini India, Mbali na maelezo ya jitihada na dhamira kubwa katika kuwekeza katika maswala ya teknolojia kupitia kampeni yao ya DIGITAL INDIA, Pia nchi imepata kuelezea dhamira yao ya kuwekeza zaidi kwa kutoa misaada ya kimasomo ( Scholarships ) kwa wale watakao kuwa wakisomea masomo yatakayo wezesha kukuza na kufanikisha jitihada zao za Digital India.

Aidha, Kwa Upande mwingine – Wameweza kukubali tatizo linalo ambatana na ukuaji wa technolojia ni uhalifu mtandao huku ikielezwa watumiaji wa simu wamefikia asilimia 97% ya raia wa nchini humo, kitu ambacho kinapelekea matumizi mtandao kuingiwa na dosari ya kipekee.

Itakumbukwa India kupitia taarifa inayosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" waziri mkuu wan chi hiyo alihimiza wananchi wake kujikita zaidi katika kutengeneza namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao ambapo pia iweze kutumika kutoa misaada kwa nchi nyingine.

Katika Kikao cha siku mbili, Kubwa la kiusalama mtandao ni dhamira kubwa ya moja kati ya washiriki wa mkutano huo kuonyesha dhamira yao kubwa ya kukabiliana na tishio la uhalifu kupitia mitandao ( Hasa Wizi wa fedha kupitia ATM) linalo tikisa mataifa mbali mbali hivi sasa.

Katika mazungumzo yangu maalum yaliyo ambatana na mahojianao na vyombo vya habari katika kuangazia dhamira yao hii ya kukabiliana na uhalifu mtandao kupitia wizi wa ATM, Nilipata kuunganisha mawazo na kujua namna gani Taifa la Tanzania tunaweza kuwekeza zaidi kukabiliana na hali hii ambayo pia ni tishio katika Mabenki yetu.


Moja ya mambo muhimu katika hili ambalo nimeona nililete nyumbani ni kuhakikisha tunaongeza aina ya tatu ya utabulisho katika miamala inayofanyika hivi sasa ya kifedha katika ATM zetu zote za mabenki yote. Hili litaongeza usalama katika miamala na pia tayari mataifa yaliyo jaribu aina hii ya suluhisho katika wizi mtandao imeanza kuonyesha matunda.


Natoa Wito kwa mabenki kuangazia hili, na pia na imani kubwa mabenki ya Tanzania yatakaa na kutafakari njia hii rafiki ya kuhakikisha miamala ya wateja wao inaweza kubaki salama ili kuongeza imani kwa wateja wao juu ya fedha zao na wao kutopata hasara kubwa inayopatikana hivi sasa kwenye miamala ya biashara kupia mashine za ATM.

No comments:

Post a Comment