WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday 30 January 2015

SIKU YA KIMATAIFA YA FARAGHA YA TAARIFA (DPD) NA YAKUZINGATIA

Mataifa mbalimbali duniani ifikapo tarehe 28 ya kila mwezi wa kwanza wanaadhimisha siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa ambapo kunakua na matukio mbali mbali ya kuhamasisha njia rafiki za kuweka salama taarifa za watu hasa wawapo mtandaoni. Taarifa zaidi za siku hii "BONYEZA HAPA"

Siku hii imekua ikitumika vizuri kwa ushirikiano mkubwa ma mashirika binafsi, serikali na vyombo vya habari kukumbusha watumiaji mitandao kuzingatia matumizi salama ya mitandao ili kubakisha taarifa za watumiaji mtandao salama.

Inafahamika, ukuaji wa wa kasi wa Teknolojia umeambatana matumizi yasiokusudiwa wa teknolojia ambapo umekua ukihatarisha sana ufaragha wa watumiaji wa teknolojia hizo. Kwa kuzingatia hili siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa imekua ikihimizwa kutumika vizuri kukumbusha watumiaji mtandao yale yanayoweza kuhakikisha taarifa zao zinabaki salama watumiapo mitandao.

Kwa uchache mambo kadhaa ya kuzingatia ili kuweza kulinda faragha yako ya taarifa ikiwa ni ukumbusho ni kama yafuatayo:-

Kupitia mahojiano maalumu katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa yaliyofanyika kati yangu na kituo cha radio cha East Africa pamepata kuanishwa kwa uchache mambo muhimu ya kuzingatia ili kuweza kujiweka salama utumiapo mtandao na kuhakiki taarifa zako zinabaki salama ambapo ni umakini wa kuperuzi tovuti pamoja na utumiaji wa Hotspots (Wifi au Wireless) zinazotolewa bure katika maeneo ya mkusanyiko.

Ufafanuzi wa kujua jinsi gani utajua kama tovuti unayoitembelea ni salama au la – Kuna tool maarufu ijulikanayo kama “WOT – Web Of Trust” ambayo inatoa msaada wa kutoa tathmini ya tovuti. Inapo ona tovuti haiku salama inakutahadharisha unapojaribu kuitembelea, ni vizuri ikatumiwa ili iweze kukupa msaada wa kujua kama unachotembelea ni salama au la.


Aidha, Ufafanuzi juu ya Man in the middle attack – Unapotumia Wifi za bure si zote zinakua ziko salama na ndio maana mara nyingi wana tahadharisha “Use it at your own risk” ikimaanisha ukiitumia basi ujue lolote linaweza kukutokea. Ili kujua kama Wireless unayoitumia iko salama hakikisha ina alama ya kikufuli au maelezo kua ni salama kinyume na hapo mtu yoyote anaweza kuona kila unacho safirisha.kujifunza zaidi  juu ya Man in the middle attack "BONYEZA HAPA"

Ikumbukwe kilichozungumzwa hapo juu ni kwa uchache tu katika mengi na pia ni vigumu kuwa salama kwa asilimia miamoja ingawa kilicho jadiliwa ni njia mbali mbali zinazoweza kuweka ugumu wa taarifa zako kufikiwa kirahisi na wahalifu mtandao.

Msisisito ni kua kila mmoja anajukumu kubwa la kuhakiki anajiweka salama binafsi na kumueka salama mwenzake. Hii ni pamoja na kuhakiki usambazi viambatanishi mtandaoni vinavyoweza kuwa hatarishi kwa wengine. Mfano: Kumekua na uhalifu mtandao unaojulikana kama “Fishing” ambapo kwa bahati mbaya baadhi ya watu kwa kutokujua wamekua wakiwasambazia wengine na hatimae kuongeza wigo la usambaaji wa uhalifu uo na hatimae wengi taarifa zao kuwa mashakani.


Aidha, bado kumekua na muamko unaokua kwa kasi ndogo wa watu binafsi kujenga tabia ya kufatilia taarifa zinazoweza kutoa msaada wa kila mmoja kuweza kubakisha salama taarifa zake atumiapo mtandao.


Nitoe wito kwa kila mmoja kuwa na tabia ya kujifunza na kutaka kujua zaidi juu ya matumizi salama ya mitandao yatakayo wezesha taarifa za kila mmoja kubaki salama.

No comments:

Post a Comment