WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Wednesday 22 October 2014

WARSHA YA MASWALA YA USALAMA MITANDAO NCHINI YA FUNZA MENGI NA KUIBUA FURSA ZA AINA YAKE

Nchi ya Tanzania imepata bahati ya kipekee kuwa mwenyeji wa warsha ya Kimataifa ya maswala ya usalama mitandao iliyo shirikisha mataifa mbali mbali kujadili na kuongezeana uwezo wa jinsi wa kukabiliana na changamoto kubwa katika maswala ya uhalifu mitandao.

Warsha hii imekuja muda muafaka baada ya taarifa niliyo iandikia "HAPA" niliyo himiza na kuonyesha umuhimu mkubwa wa kuunganisha nguvu za pamoja kwenye vita dhidi ya uhalifu mtandao ikizingatiwa uhalifu mtandao ni uhalifu usio mipaka na kuna mahitaji makubwa ya kushirikiana katika taarifa na utaalam.

Warsha hii imekua na mafanikio makubwa sana ambapo nikiwa kama mtaalam wa maswala ya usalama mitandao na uchunguzi wa makosa ya digitali naweza kusema ni mengi tumeweza kubadilishana na uwezo  wa kuendeleza mapambano zaidi dhidi ya uhalifu mtandao umeongezeka kwa washiriki wote.

Wito Mkubwa ulitolewa na katibu mkuu wa wizara ya sayansi mawasiliano na teknolojia nchini profesa Patrick Makungu kuwataka wataalam na washiriki wengine kutochoka na kuongeza jitihada kukabiliana na wimbi la uhalifu mtandao linalokua kwa kasi duniani kote ili kuweza kuwa mbele ya wahalifu mitandao kupitia hotuba aliyo isoma kwa niamba ya Waziri wa Wizara  hiyo kama inavyoweza kusomeka "HAPA"


Aidha, Mkurugenzi mkuu wa COSTECH, Dr. Hassan Mshinda alifafanua umuhimu wa warsha na kueleza nifursa nzuri sana kwa watanzania na kuanisha ni mikakati endelevu yakuendelea kukuza uwezo wa wataalam wa ndani. Mimi binafsi pia nilipata kujadili namna ya kukuza ushirikiano na wageni hao katika eneo hili muhimu la usalama katika mitandao.


Mwezi Octoba pia umeaswa kutumika vizuri ili kuweza kuhakiki uelewa wa maswala ya usalama mitandao kwa watumiaji umeweza kufanyiwa kazi huku pakiainishwa jitihada mbali mbali za serikali ya Tanzania inayo endelea nazo kuweza kukabiliana na wimbi la uhalifu Mtandao nchini.

Taarifa hii imeweza kuandikwa kwa kifupi kwa lugha ya kingereza kama inavyoweza kusomeka kwenye gazeti la "DAILYNEWS"

JOPO LA WANANDAAJI KUTOKEA WA WARSHA YA USALAMA MITANDAO KUTOKEA COMSAT WAKIBADILISHANA MAWAZO NAMI   KUPANGA MIKAKATI ENDELEVU NA RAFIKI KUONGEZA UWEZO KWA WATAALAM WA NDANI

No comments:

Post a Comment