WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday 18 September 2014

OKTOBA NI MWEZI WA KUKUZA UELEWA WA MATUMIZI SALAMA YA MITANDAO


Miaka 11 iliyopita Marekani ikitambua ukuaji wa matumizi mabaya ya mitandao walianzisha kampeni maalum iliyoamuliwa kufanyika kila mwezi oktoba. Kampeni hiyo maalum ilihamasisha mashule , kampuni binafsi na  serikali kutumia mwezi oktoba kuhamashisha uelewa wa matumizi salama ya mitandao.

Kadri muda ulivyojongea Mataifa mengine yaliamua kutumia mwezi huo kuwa mwezi wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao ambapo sasa mataifa mengi tayari yamesha kua yakiazimisha kampeni hizi. Mwaka huu wa 2014 Kama Inavyo ainishwa "HAPA" imeweza kuchanganua  kwa ufupi  maudhui na kauli mbiu ya mwaka huu, ratiba, namna ya kushiriki na mambo mengine muhimu.


Ifahamike vizuri jitihada za kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao duniani kote ni endelevu na mwezi oktoba umechukuliwa kuwa maalum ili kuonyesha umuhimu wa kampeni hizi kwa kuzingatia ukuaji wa matumizi ya mitandao unaoambatana kabisa na matumizi mapaya kwa baadhi ya watu.

"JUMBE"  teule kwa upande wangu ni kuongeza matumizi mazuri na sahihi ya maneno ya siri ili kujiweka salama utumiapo mitandao.

Kwa Upande mwingine Tanzania imeendelea kuwa mwenyeji wa midahalo na  warsha mbali mbali zihusianazo na maswala ya usalama mitandao ambapo ni fursa nzuri kwa watanzania kuweza kushiriki ili kukuza uelewa wa maswala haya ya ulinzi mitandao ambapo dunia ya leo yemeonekana kua na sura ya pekee.


Mwanzoni mwa mwaka huu Nikiwa Ughaibuni, Kwenye "MKUTANO"mkuu wa mwaka katika maswala usalama mitandao na teknolojia ya habari kwa ujumla miongoni mwa mazungumzo mengi nje ya vikao yalionyesha mataifa mbali mbali kua na jitihada binafsi za kuhakiki mikutano na warsha mbali mabli zinachukua nafasi ya pekee ili kuhamasisha matumizi salama  ya teknolojia habari na mawasiliano.

Kwa Tanzania, "MKUTANO" Unaotegemea kukamilika Hapo Kesho wa Maswala Ya Usalama Mitandao Jijini Arusha umekua ni moja ya fursa nzuri kwa watanzania kuhakiki wanatambua hali halisi kuhusiana na uhalifu mtandao na jitihada endelevu zinazoendelea kwenye taifa kwenye mapambano dhidi ya uhalifu mtandao.

Aidha, mwezi wa Oktoba  mwaka huu Tanzania Inategemewa kuwa mwenyeji wa mkutano/ Warsha ya kimataifa ya maswala ya usalama katika mitandao ambapo wataalam kutoka mataifa mbali mbali watategemewa kujadili maswala mbali mbali. Kushiriki warsha hii muhimu,Mtanzania anapaswa kusoma na kujaza Fomu maalumu iliyo ambatanishwa hapo chini na kuirudisha COSTECH Tanzania.


Mwezi Novemba mkutano Mwingine mkubwa wa kufunga mwaka unaotegemewa kuhusisha wataalam mbali mbali wa maswala ya uslama mitandao watakutana kuongezeana uwezo na kujadili maswala makuu manne ya jinsi ya kutambua uhalifu mtandao, Kuuzuia, Kuchukulia hatua unapotokea na jinsi ya kurudisha uslama mitandao katika hali yake ya awali baada ya kutokea.

"MKUTANO" huu ambapo Mwenyeji wake ni Nchi ya Afrika Kusini ni fursa nyingine kwa watanzania kuhuduria ili kujua mengi katika maswala haya ya uhalifu mitandao ikizingatiwa mimi nikiwa kama Mtanzania kuteuliwa kuwa katika Paneli ya Washauri katika Mkutano huo.

1 comment:

  1. N.B: The article is in SWAHILI But, The attached Links are In ENGLISH.

    ReplyDelete