WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday 7 August 2014

TEKNOLOJIA YA MIWANI YA KISASA YAWA TISHIO

Kumekua na wimbi la ukuaji wa teknolojia kila kukicha, Ukuaji huu wa teknolojia umepelekea matumizi makubwa ya mitandao maeneo mengi na hili linaenda sambamba na ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao hivi sasa. Mbali na "MIWANI" pamoja na "MAGARI YASIYO NA DEREVA" kutoka Google, pia kumekua na aina nyingine ya miwani maarufu kama “Spy glasses” ambayo awali iliaminika inatumiwa zaidi na wahalifu ( wadukuzi) wa taarifa za watu.

Miongoni mwa maswala yaliyo umiza vichwa wataalam wa maswala ya usalama mitandao katika mijadala ni pamoja na kupima athari za miwani hii ya kisasa ambayo inakua imeambatanishwa na kifaa chenye uwezo wa kuona, na kusafirisha taarifa upande wa pili huku pande zote mbili kuweza kusafirisha sauti kupitia mawani hiyo.

Aina tatu za mawani hizi za kisasa ziliweza kuangaziwa macho na wataalam wa maswala ya usalama mitandao ili kujua ni athari kiasi gani zinaweza kuleta kwa jamii na badae katika kampeni ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao kwa msaada wa tasnia ya uigizaji, Hollywood kupitia Tamthilia ya "NIKITA" kwenye kipengele chake cha mwisho sehemu ya kwanza naya tatu walitolea ufafanuzi aina mbili za miwani na uwezo wake.

Aina hiyo ya mawani sasa imeonekana kuchukua sura mpya pale Polisi nchini uchina kukamata wanafunzi waliyokuwa wakitumia miwani hiyo wakati wakifanya mitihani ilikuwasiliana na walio nje kupatiwa majibu ya mtihani. Uchunguzi huo uliambatana na tahadhari kuwa miwani hiyo iko kawaida sana na kwa haraka haraka si rahisi kuitambua hivyo wasimamizi mitihani kutakiwa kuwa makini sana kwa wavaaji miwani.


Aidha, aina hii ya miwani pia imehofiwa kuenea zaidi ambapo inaaminiwa kwa kushirikiana na teknolojia ya simu zinazo tumiwa na wahalifu kufatilia watu kwa pamoja zinategemewa kutumiwa vibaya na hatimae kusababisha wimbi la uhalifu mtandao lililoboreshwa zaidi kuleta madhara makubwa kwa mataifa mbali mbali.

No comments:

Post a Comment