WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Tuesday 15 July 2014

ANGALIZO KWA WATEJA WANAOFANYA MIAMALA YA BIASHARA KUPITIA MITANDAO

Huduma ya kufanya miamala ya kibiashara kupitia mtandao inafanya maisha ya leo kua rahisi zaidi kulinganisha na maisha ya awali. Hii ni kutokana na uwezekano wa kufanya miamala hiyo popote pale ilimradi tu uwe unamtandao.

 Hili lakua na mtandao kwa Tanzania limeendelea kuwa rahisi hasa baada ya mitandao ya simu kutoa huduma za wavuti inayo sababisha takriban watanzania walio wengi hasa waishio mijini kuweza kupata huduma za mitandao.

Kila teknolojia inachangamoto zake. Na hii ya kufanya miamala kwa msaada wa mtandao pia imekuja na changamoto kadhaa ambazo bado kuna tatizo kubwa la uelewa wa jinsi gani ya kua salama pale miamala ya kibiashara inapofanywa.

Muamala wa kibiashara unapofanyika vibaya unaweza kumgharimu sana mtumiaji  kwa kupoteza fedha na hata kupoteza utambulisho wake ( Hii ni pale taarifa zako kupatikana na wahalifu na kutumika vibaya baadae).

Swala la uhalifu mtandao unao athiri miamala ya kibiashara inayofanywa kwa msaada wa mitandao hapo awali ulikua maarufu sana katika nchi za afrika magharibi hasa Nchi kama Nigeria  na Ghana – Unaweza kusoma taarifa ya nchi hizo na hali ilivyo hadi sasa kupitia taarifa inayosomeka "HAPA"


Aidha Kwa afrika mashariki ikiwemo Tanzania, Hali Imebadilika na Hivi sasa uhalifu huu umeendelea kushika kasi sana ambapo wahalifu mtandao wamekua wakielekeza zaidi nguvu zao kuibia watu wafanyao miamala ya kibiashara kwa msaada wa Mitandao. Hivi karibuni nilipata kuandikia taarifa ya uhalifu mpya unaokua kwa kasi kama inavyosomeka "HAPA" nikifafanua hali halisi nchini hivi sasa kwenye hili.

Hivi karibuni Benki ya CRDB imewaonya wateja wake kuwa makini na baadhi ya mitandao inayoibuka na kulaghai kwa kuwataka wananchi,kutoa taarifa zao muhimu za kibenki,jambo ambalo linahatarisha usalama wa fedha zao zinazohifadhiwa na benki hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dr Charles Kimei alipolizungumzia hili jijini Dar es salaam alifafanua kuwa kumeibuka mchezo kwa baadhi ya mitandao ya kijamii,ikijaribu kuwalaghai wateja kwa kuwaomba taarifa za akaunti zao ili kufanya uhalifu.

Alisisitiza wananchi wanatakiwa kuwa makini na kundi hilo,wasikubali kudanganyika kwa kutoa taarifa zinazohusiana na nyaraka nyeti za benki zao na kusisitiza kuwa ni marufuku kutoa taarifa hizo kwa wafanyakazi wa benki.

Mkurugenzi huyo amesema pamoja na kwamba benki hiyo inawapigia simu wateja wao wakitaka kukamilisha usaili wao kuhusiana na kuingia katika mfumo wa uboreshaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi unaoitwa Simbaking  watambue kuwa hawataulizwa kutoa taarifa zozote za akaunti.

Kuhusu mbinu zinazotumiwa na wahalifu,Mkurugenzi wa Idara Hatarishi James Mabula amesema huwapigia simu wakijifanya kuwa wakurugenzi ama wafanyakazi wa benki hiyo na kisha kuwaghilibu kwa kutaka kupatiwa namba za siri za akaunti husika.

Kwa upande mwingine, Mitandao ya simu bado haijabaki salama – huduma za  miamala inayofanywa kwa msaada wa simu pia imeendelea kuathirika ambapo kila mara pameendelea kuripotiwa uhalifu katika maeneo hayo.


Nilipata kuandika mwishoni mwa mwaka jana Taarifa ya kingereza inayosomeka hapo chini kuonyesha hali halisi na makabiliano yanayoendelea kudhibiti uhalifu huu mtandao nchini Tanzania huku nikiambatanisha na mapendekezo ambapo juhudi za dhati kuyaendea zinaendela ili kupata taifa salama kimtandao.

No comments:

Post a Comment