WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Monday 9 June 2014

KENYA KUANZISHA KITENGO MAALUM CHA KUPAMBANA NA UHALIFU MTANDAO

Bwana. Keriako Tobiko
Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma ya nchini Kenya Bwana. Keriako Tobiko ametangaza kuanzishwa kwa kitengo maalumu kitakacho pambana na  uhalifu mtandao katika ofisi yake. Amedai hatua hii imefikiwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya uhalifu unaofanywa na wahalifu wenye uelewa wa teknolojia.

"Kwa mtazamo wa kuongezeka kwa uhalifu wa mtandao, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Umma (ODPP) imeanzisha kitengo maalumu kusimamia mashtaka ya wahalifu wa mtandao," Tobiko alisema, kwa mujibu wa The Standard la Kenya.

Takwimu zinaonyesha Kenya inapoteza kiasi cha shilingi bilioni 2 (Dola milioni 23.3) kwa mwaka kupitia uhalifu wa mtandao." Aliongeza Bwana Tobiko.

Hata hivyo, alisema, jitihada za kuwakamata na kuwashitaki watuhumiwa zimekua ngumu kutokana na ukosefu wa sheria zinazofaa, zikiwaacha huru wahalifu kufanya uhalifu wa mtandao ambao unatishia usalama wa taifa, miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na haki ya usiri wa raia.


"Kwa kutambua kwamba kwa sasa kuna sheria zisizotosheleza za kushtaki uhalifu wa mtandao, ODPP imeandaa warsha ya kupitia upya sheria zilizopo na kuandaa rasimu ya mswada wa kina kuhusu uhalifu wa mtandao kulingana na taratibu husika za kimataifa zinazofaa," Tobiko alisema, akiongeza kwamba matumaini ya kuwa na mswada wa kina wa uhalifu wa mtandao yatakamilika mwaka huu.


Itakumbukwa taarifa iliyo andikwa na  tovuti ya sabahi inayosomeka "HAPA" iliainisha nchi ya Kenya imekua ikikabiliwa na idadi kubwa ya uhalifu kwa kutumia zana za teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo uhalifu kuanzia ngazi ya wizi kuwaibia watumiaji wa simu hadi viwango vya juu vya udanganyifu unaozigharimu taasisi za fedha mamilioni ya dola imeendelea kushamiri.

Baadae shirika la Umoja wa Mataifa la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) lilieelezea wasiwasi wake kuhusu mifumo ya usalama wa mitandao na hatimae ITU ilisaini makubaliano na Tume ya Mawasiliano ya Kenya (CCK) ya kuboresha ujuzi wa watu wanaofanyakazi na Timu ya Kushughulikia Matukio ya Kompyuta.

Kwa Upande wa Tanzania changamoto iliyokua ikirudisha nyuma juhudi za kupambana na uhalifu mtandao imepatiwa suluhu baada ya kuwepo kwa kitengo maalum cha kupambana na uhalifu mtandao ambacho kimejiri kwa muda sasa huku kikitegemewa kuwa na ufanisi zaidi  kutokana na kukamilika kwa rasimu itakayowezesha waalifu kushughulikiwa kisheria. Taarifa kuhusiana na hili inasomeka "HAPA"

Aidha tukiangalia afrika kasi ya mapambano imeongezeka huku Afrika ya kusini ikifanikiwa kubomoa kikundi cha wahalifu mtandao waliokua wakiathiri sana nchi nyingi – Taarifa hiyo ya afrika kusini inasomeka "HAPA" Rwanda nao hajabaki nyuma kasi ya kuendana na ulimwengu wa “DOT” com pamoja na kuongeza nguvu kupambana na uhalifu mtandao imeonyesha kuchukua sura mpya – Taarifa ya hili inasomeka "HAPA"

Napenda kumalizia kwa kutolea mfano wa Ghana kupitia taarifa inayosomeka "HAPA"na kuendelea kutoa wito kwa wananchi kutambua ya kua swala la uhalifu mtandao linakua sawa kabisa na teknolojia inavyokua na changamoto za mapambano ni kubwa kama inavyosomeka "HAPA" huku tukiwa nanguvu watu wachache sana kuhimili changamoto hizo hivyo mafunzo zaidi yanaendelea kutolea maeneo mbali mbali na hili litaenda sambamba na kila mmoja kujenga tabia ya kujifunza maswala ya husuyo namna ya kujiweka salama kimtandao walau kwa uchache .

No comments:

Post a Comment