WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Friday 2 May 2014

TAHADHARI: WATUMIAJI WA TELEVISHENI ZA PHILIPS WAKO HATARINI



Ni ukweli matumizi ya mtandao ni swala lisilo epukika katika kufanya mambo mbali mbali ya kila siku ikiwa ni pamoja na kufanya miamala ya biashara, mawasiliano, kuhabarisha na mengineyo.Taarifa ya awali niliyo iandikia kuhusiana na ukuwaji wa matumizi mtandao na athari zinazoendelea kukua inaweza kusomeka hapa “TANZANIA NA HALI YA USALAMA MTANDAOtaarifa iliyo weza kusomwa na kituo cha radio cha “CLOUDS FM” na kuandikwa kirefu kupitia “MWANANCHI

 Tishio jingene jipya la kiusalama mtandao limebainishwa kwa watumiaji wa televisheni za Philips toleo la la mwaka 2013 maarufu kama “Philips smart TVs” ambapo wahalifu mtandao wanauwezo wa kuingilia TV hizo na kuanza kurusha matangazo yao binafsi  pamoja na kufatilia kila kinacho tazamwa na mtumiaji.

Tahadhari hii imetolewa ikiambatana na ushauri ambapo imeelezwa wahalifu mtandao wanauwezo mkubwa sana wa kuleta athari kwa watumiaji wa televisheni hizo na msemo “You have been watched” unaomaanisha unatazamwa kuanza kutumika kwenye mitandao ya kijamii kuelezea hisia za waathirika.



Tayari Kampuni ya Philips imekiri kuwepo kwa tatizo na kueleza kampuni hiyo ipo katika jitihada za dhati kulitatua tatizo huku ikiwataka watumiaji wa Aina hii ya TV kuzima Kinachijulikana kama “Miracast function” amapo hili linaweza kufanyika kwa kufata maelekezo yafuatayo (Quick help: Press the HOME button –  navigate to Set up – select Network Settings –  Select Miracast – set to OFF). Kukiri kwa tatizo katika lugha ya kingereza inaweza kusomeka “HAPA

VIDEO INAYO ONYESHA  UHALIFU UNAVYO FANYIKA.

No comments:

Post a Comment