WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Monday 17 February 2014

HALI YA USALAMA WA KIMTANDAO - 3

Sehemu ya pili Wiki Iliyo pita nilizungumziwa kipengele cha Tatu, kuhusu barua pepe, kuna wimbi la wahalifu mtandao ambao wanatumia anuani za watu na mitandao mingine ya kijamii kuandika kwa watu wasiowajua ama kueleza wanahitaji urafiki au wako katika mazingira magumu hivyo wanahitaji msaada fulani kutoka kwako. Usijibu barua kama hizi, kwani chochote utakachojibu kinaweza kukuingiza matatani.
Kuna kitu kitaalamu kinaitwa “Reconnaissance” ambapo ni hatua mojawapo inayotumiwa na wahalifu kukusanya maelezo ya watu wanaotaka kuwadhuru.
Muendelezo wiki hii katika sehemu ya nne, Matumizi Ya ATM, Kua makini sana na mtu anae kuomba kuhamisha fedha zake kwenyye account yako ya benk ili aweze kuitumia account yako kutoa fedha hizo kwani kwa sasa wahalifu mtandao katika maeneo haya ya Wizi katika ATM wamekuja na njia hii ambapo wanatengeneza mazingira ya uhitaji wa msaada wako kwa kukuuomba wakutumie fedha ili account yako itumike kuzitoa huku wakijua wao watakua salama na wewe Unaetumika account yako unaingia matatani bila kujua kwani maranyingi hali hii inakua inahusisha pesa za wiizi. na Kwa sasa Wizi wa aina hii umekua ukija kwa kasi na wengei ambao kwa namna moja au nyingine huwenda hawakujua kua ni tatizo na mara baada yakutoa msaada huu wanajikua wameingia katika hatia ya kujibu mashtaka ya wizi Mtandao.

Tano, Website Feki, Kwa sasa Takwimu imeongezeka sana ya websaiti Feki Ambbapo Tumeliona hili katika mapitio ya Makosa ya kimtandao yajayo kwa kasi katika kikao kilichofanyika Jijini nairobi mapema mwezi wa sita mwaka huu. Ambapo Kumeonekana watu wamekua wakitengeneza website ambazo zinakua zinafanana na za mabenk ambazo unapo ingia kwa ajili ya kufanya "Online Transaction" unaweza kujikuta umeweka details zako ambazo ni pamoja na Paswed yako kwenye Website feki ambapo Baadae wahalifu mtandao wanakusanya taarifa hizo kwa matumizi ya wizi wa fedha. Lakini pia Inaweza ikawa ni katika website za kawaida za social media ambapo kikubwa ni kufanya uingize details zako katika website feki yenye kufanana na uliyo izoea na mara baada ya kufanya hivyo tayari wanakua wamepata wanacho kihitaji.

Kwenye hili Kuna Somo Refu kiasi ambalo linaweza kutoa ufahamu jinsi gani utaitambu website ambayo si halali (Feki) Nategemea kulitoa karibuni. Naimani litatoa muono kwa watu ili kkuweza kua makini zaidi baada ya utambuzi. Pia Kwenye hili Kumekua pia na wimbi la watu wamekua waki tengeneza accounts za mitandao ya kijamii kwa kuiga mtu mwingine kisha kutumia watu urafiki kwa nia za kuiba taarifa za mtu muhusika. ni vizuri pia tukawa makini kwenye hili.


Napenda kuhitimisha kwa kusema, Sikuzote unapokua katika mitandao unakua si salama hivyo kunanjia nyingi ambazo wenzetu katika nchi mablii mbali wamekua wakionyesha jitihada waau kupunguza hali ya kua hatarini uwapo mitandaoni kwa ku weka taratibu mbali mbalii ambapo kwa sasa tanzania pia itakua ikijittahidi kuweka taratibu hizo na pia kutoa mafunzo ya ufahamu kwa wananchi ili kupunguza hali hii ya Makosa Ya Kimtandao ambapo yanakua kwa kasi sana shivi sasa.

No comments:

Post a Comment