WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Saturday 4 January 2014

ANGALIZO KWA WATUMIAJI WA WINDOW XP

Kampuni ya Microsoft imetoa angalizo kwa wateja wake ambao bado wanatumia “Window XP”. Kampuni hiyo imeeleza kuwa hapatakuwepo na “updates” zaidi kwenye “Window XP Service Pack 3” baada ya mwezi wanne mwaka 2014.
Akiongea na wataalam mbali mbali wa maswala ya ulinzi mtandao August 16 Mwaka 2013, Bwana Tim Rains alisema “Ingawa Window XP wakati imetolewa ilikua ni yenye ubora na yenye kupendwa zaidi,  kwa sasa imekua ni dhaifu  kutokana na ongezeko la uhaifu mtandao”

Aliongeza na kusema Mara baada ya kuacha kuendelea kuihudumia Window XP wahalifu mtandao “Hackers” watatumia mianya hiyo kuweza kuingilia Komputa za wateja wao ambao watakua wanaendelea na matumizi ya Windo XP huku akiendelea kusisitiza Windows mpya ambazo zimekua ziki endelea kutolewa na Kampuni hiyo Ya Microsoft zimeendelea kutafutiwa suluhu pale tu inapo onekana wahalifu mtandao wameweza kugundua namna ya kupenyeza na kuweza kuingia katika Komputa za watu bila ridhaa yao bodhaa zao za Microsoft.

“Kwa sasa Microsoft Security Response Center imekua ikotoa “Updates” kwa wateja wao ili kuwalinda dhidi ya wahalifu wenye nia ya kupenya kwenye komputa zinazotumia bidhaa zao. Ifikapo tarehe 8 ya Mwezi wa Nne mwaka Huu wa 2013, Makampuni ambayo bado yatakua yanatumia Window XP wahalifu mtandao “Attackers” wanaweza kuwa na namna ya kutafuta mapuungufu katika Window XP ambapo baadae wanaweza kutumia mapungufu hayo kuleta athari na Kampuni ya Microsoft haitakua na usaidizi wa bure au wa kulipia ndidi ya hali hiyo kwani tayari itakua imekwisha acha kutoa msaada dhidi ya Window XP” alisema bwana Tim Rains.

Wachangiaji wa mada hiyo waliweza kuonyesha Hisia tofauti dhidi ya angalizo hilo, Na tulipo zungumza na bwana Yusuph Kileo ndidi ya Taarifa hiyo alisema, “Naimani kabisa Tarehe zitafika nabado baadhi ya Makampuni yataendelea na matumizi Ya Window hiyo ambapo huwenda ikaongeza urahisi wa wahalifu kupenyeza katika mifumo mbali mbali inayo tumia window Hiyo ya XP ingawa Microsoft tayari wamesha tangaza ya kua msaada zaidi katika Window XP hautakuwepo na huwenda ikawa ndio sababu ya wahalifu kuanza kutumia mwanya huo kuingilia Komputa za watu wenye matumizi ya Window hiyo ya XP”

Aidha kwa taarifa nyingine, Tarehe 19 Ya Mwezi wa nane 2013 Jijini California Nchini Marekani Jaji Charles Breyer wa mahakama ya Wilaya jijini humo ametoa hukumu kwa watumiaji wa mitandao ambao wamekua na tabia ya kubadilisha IP (internet protocol) au kuwa na matumizi ya “Proxy server” kwa malengo ya kuzingilia Tovuti nyingine “Public Websites”.
Katika kesi hiyo iliyo husisha makampuni mawili ya nchi hiyo yaliyo jilikana kama “Craigslist” pamoja na “3taps” Jaji huyo Alifafanua kwa kusema mtumiaji anapokua na tabia hiyo atakua amekiuka kipengele cha katiba ya nchi hiyo kinachojulikana kama CFAA “Computer Fraud and Abuse Act”.

Alipo ulizwa bwana Yusuph Kileo kuhusiana na tukio hilo alizungumza na kusema “Kilichotokea katika kesi hiyo ni kwamba 3taps wali ingia kwenye Kampuni ya Craigslist kwa kubadilisha IP(Internet Protocol) yake na kutumia “Proxy server” ili kuficha utambulisho wake “Identity” huku wakichukua taarifa kutoka katika kampuni ya Craiglist  ndipo Graiglist walipo fungua mashtaka dhidi ya kampuni ya 3taps.



Baadae jaji ndipo alipo toa hukumu kenye kesi hiyo aki nukuu moja ya sheria ya nchi hiyo inayojulikana kama CFAA” ambapo Sheria hiyo inaelekeza kuingia hatiani kwa yeyote atakae ingilia Komputa ya mwingine bila ridhaa na kuchukua taarifa zozote.
Sheria hiyo ni ya “18 USC § 1030 - Fraud and related activity in connection with computers” kipengele cha (a) (2) (c) inayo eleza “Whoever intentionally accesses a computer without authorization or exceeds authorized access, and thereby obtains information from any protected computer . . . . ”  

Aidha Bwana Yusuph Kileo Alieleza jambo jingine ambapo anategemea kumpokea mgeni ambaye ndie Mmiliki wa Wolfpack Security na  Director wa SANS- Africa pia ni  Mwenye kiti wa Kundi Linalojihusisha na Ulinzi mtandao katika Nchi za Africa ambapo yeye ni mwanachama wake wa kudumu. Mgeni huyo anategemewa kuwasili Nchini jioni ya tarehe 12 September 2013 na Kuondoka Nchini Tarehe 13 September 2013.

Aidha bwana Yusuph Alieleza Mgeni huyo Anategemewa kuhudhuria Chakula Cha jioni na Wataalam wa Tanzania katika Fani ya TEHAMA Ambapo watapata fursa yaku badilishana mawazo.
Pia anategemewa kutoa mafunzo mafupi siku inayofatia na kasha kupata kuzungumza na baadhi ya Wadau nchini ili kuweza kubadilishana mawazo kuhusiana na hali ya uhalifu mtandao katika ngazi ya afrika na Dunia Kwa Ujumla.

Itakua Ni fursa kwa wataalam wa kitanzania Kuweza kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na mtu huyu adimu ambae amekua mwandalizi na mfunguzi mikutano  inayo wahusisha waatalaam wa maswala ya ulinzi mtandao na Uchunguzi wa makosa yadigitali ambaye pia ni mwanachama  wa Wataalam wa ulinzi mtandao na Uchunguzi wa makosa ya Digitali Duniani.

Source: Mwananchi Jumanne August 27 2013.

No comments:

Post a Comment